Published On: Thu, Jun 4th, 2015

BG TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UFANYAJI USAFI WA MAZIBNGIRA.

Share This
Tags

Katika kuadhimisha wiki ya mazingira duniani, Kampuni  ya uchimbaji wa gesi asilia na mafuta BG Tanzania,  imekabidhi vifaa vya kuzuia na kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, vyenye thamani ya shilingi milioni 146, kwa Hifadhi ya bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma (Marine Park), ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza katika sherehe fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mtwara TAIFORD NDOMBA amesema, kitendo cha BG Tanzania kuhamasisha juu ya upandaji miti hasa kwenye mashule ni kitu kizuri na cha kuigwa na watanzania.

Kwa upande wake Mhifadhi Mfawidhi wa Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma, REDFRED NGOWO, amewashuruku BG Tanzania kwa kuwakabidhi vifaa ambavyo vitawasaidia kuondoa mafuta baharini, pindi ajali za meli zinapotokea.

BG Tanzania ilihamasisha upandaji wa miti katika shule za msingi 14, tatu kati ya hizo ni za sekondari, zilizopo kwenye ukanda wa bahari ya Hindi Mtwara Vijijini, ili ziweze kulinda utunzaji wa mazingira huku baadhi ya shule zikipatiwa zawadi ya ushindi, wa utunzaji miti na kampuni hiyo.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>