Published On: Tue, May 26th, 2015

TCRA KUWASHINDANISHA WATOA HUDUMA YA MAWASILIANO.

Share This
Tags

SEKTA ya mawasiliano ni moja ya viungo muhimu katika harakati za nchi yoyote ile Duniani kujiletea maendeleo, hii ni kutokana na ukweli kuwa siku za hivi karibuni sekta hiyo imeweza kusaidia kutoa urahisi kwa wananchi kutoka eneo moja hadi jingine kupitia mawasiliano.

Lakini kampuni gani inapaswa kupewa kipaumbele kuuziwa masafa yenye nguvu ili kutoa huduma zao kwa ufanisi ni jambo ambalo Mamlaka ya Mawasiliano TCRA limekuwa likiumiza kichwa kwa muda mrefu hatua iliyowalazimu kuanzisha mnada wenye lengo la kuwashindanisha watoa huduma hao kulingana na vigezo vyao.

Mnada ni jambo lolote linalowawezesha wanunuzi kushindana kwa kuzingatia vigezo, je hatua hiyo kwa upande wa masafa italeta tija ipi kwa watoa huduma hao..

Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Afrika ya Makampuni ya simu za mikononi zinazotumia mfumo wa GSM Mortimer Hope amesema utaratibu huo wa mnada huku mmoja wa washiriki wa mkutano huo akizungumzia hatua hiyo.

Aidha MORTIMER amesema kuanza kutumika kwa utaratibu huo hapa nchini kwa kiasi kikubwa utasaidia kuleta ushindani wa kweli kwa watoa huduma na hivyo kuharakisha kasi yta ukuaji wa maendeleo kupitia sekta ya mawasiliano

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>