Published On: Mon, May 25th, 2015

MRADI WA VIWANJA VYA BEI NAFUU MKOMBOZI KWA WANANCHI NA BAYPOT

Share This
Tags

Hivi karibuni jiji la Dar es salaam lilipata mvua kubwa ambazo zilisababisha mafuriko makubwa hasa kwa wale wakazi wanaoishi mabondeni .

Baada ya kuiona kero hio taasisi ya kifedha ya BAYPOT imeaandaa mpango maalumu wa kuwauzia viwanja kwa bei nafuu wakaazi wa maeneo mbali mbali kwa njia ya kuwaepusha na adha ya kuvamiwa na mafuriko ya mara kwa mara.

Akiongea katika uzinduzi wa mradi wa viwanja hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa BAYPOT JOHN MBAGA amesema viwanja hivyo vilivyoko kibaha vitaweza kuwasaidia kuwaondolea adha watu wanaoishi mabondeni ndio sababu wametenga baadhi ya viwanja vinavyouzwa kwa nafuu.

Nae mgeni rasmi wa uzinduzi huo Afisa mipango wa Wilaya ya kibaha OBEID KATONGE amesema hakuna haja kwa wakaazi wa jijini wanaoishi mabondeni kungangania kuishi huko kutokana na viwango vilivyowekwa katika mradi huo kuweza kununuliwa na kila mtu huku eneo hilo likitengewa huduma zote za kijamii

 

Mradi huo wa viwanja vilivyopo vikuruti kibaha vimepimwa viwanja zaidi ya efu moja mianane .

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>