Published On: Sun, Mar 1st, 2015

NCHI ZA AFRIKA BADO ZINAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA MABADILIKO HALI YA HEWA

Share This
Tags

Nchi za Afrika bado zinakabiliwa na changamoto kubwa katika kukabiliana na  mabadiliko ya hali ya hewa, hali inayochangia madiliko ya mifumo ya kilimo,Ongezeko la kina cha bahari na magonjwa.

Wataalamu wa hali ya hewa nchini wamebainsha hayo katika mkutano unaowakutanisha wataalamu na wadau wa hali ya hewa kutoka nchi za Afrika unaofanyika jijini Arusha.

Akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu wizara ya uchukuzi Shaban Mwinjaku amesema kwa sasa nchi za Afrika zinafanya kila liwezekanalo katika kupunguza matumizi ya hewa ukaa,Tanzania ikiwemo.

Akizungumzia  mikakati inayofanywa na  serikali ya Tanzania katika kutekeleza mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa,mkurugenzi wa mazingira ofisi ya makamu wa Rais Dr JULIUS NINGU amesema kwa sasa serikali inafanya kila liwezekanalo kupunguza ruzuku kwenye vifaa vya gesi ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kutumia bidhaa hizo.

Katika mkutano huo mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi IPCC umekabidhi ripoti ya tano ya mapendekezo ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo kwa nchi za Afrika inakadiriwa kuzalisha hewa ukaa kwa asilimia 3 huku kiasi kikubwa kikizalishwa nchi zinazoendelea.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>