Published On: Fri, Feb 27th, 2015

WATANZANIA TUUNGANE KWA PAMOJA TUPINGE MAUWAJI YA ALIBINO

Share This
Tags

Mwaka 2009 Serikali iliendesha kura za maoni katika kanda saba ili kuwabaini watu wanaojihusisha na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, ambapo katika kipindi hicho tu pekee walemavu 43 waliuawa.

Miaka sita baadae, kipindi kama hiki kinachokaribia uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani vitendo vya mauaji ya walemavu wa ngozi vimejirudia tena huku ripoti kuhusiana na waliotajwa kwenye ripoti ya kura za siri wakiwa hawajachukuliwa hatua yoyote hadi leo.

Katika kupinga mauaji ya albino Mkurugenzi wa Msama Promotion ALEX MSAMA amehoji ukatili huo dhidi ya walemavu hao na kutoa rai kwa Serikali.

Katika hatua nyingine MSAMA ametoa msaada wa Shilingi Milioni Saba kwa Vituo vitano vya watoto yatima ikiwemo Mwandaliwa, Honoratha na Malaika ili usaidie kulipia ada za shule kwa watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo hivyo.

Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ni lazima yakomeshwe kwa namna yoyote ile, kwani kutafuta utajiri kwa kuua ndugu zetu ni aibu, ni fedheha, ni ushetani usiovumilika. Tuungane kupinga mauaji ya Albino kupitia kampeni ya MIMI NITAKULINDA.

Posted By

Displaying 1 Comments
Have Your Say
 1. hey says:

  Taxi moto line
  128 Rue la Boétie
  75008 Paris
  +33 6 51 612 712  

  Taxi moto paris

  Spot on with this write-up, I honestly feel this web site needs much
  more attention. I’ll probably be back again to read more, thanks for the advice!

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>