Published On: Fri, Feb 6th, 2015

VIJANA WAJISHUHULISHA NA UFUGAJI SAMAKI

Share This
Tags

By Iddi Nidudu:

 

Vijana wengi hasa wasio na ajira nchini wameanza kujishughulisha na ufugaji wa samaki, hivyo Wakulima wa wilaya ya Igunga mkoani Tabora wameaswa kutoudharau, kwa vile ni njia mojawapo ya kuwaingizia kipato cha kutosheleza mahitaji yao kwa muda mfupi.

Wakiwa katika mafunzo ya ufugaji samaki yanayofanyika mjini Igunga, imeonekana kuwa mfugaji samaki ataweza kupata kipato kikubwa katika eneo dogo, huku gharama za kuwalisha samaki zikiwa ni ndogo.

Wakizungumza na CLOUDS FM wakulima hao wanaochukua mafunzo ya siku saba, hawakusita kukiri kwamba yatabadili maisha yao.

Aidha afisa mfawidhi wa kituo cha ufugaji samaki Kanda ya Kati, CHARLES KALUMBETE, ameeleza manufaa anayoweza kuyapata mkulima kwa kufuga samaki.

Kituo hicho cha Serikali kilicho chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kinahudumia Mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora ambapo kwa sasa kinashughulika na samaki aina ya Kambale na Sato.

Posted By

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>